Simulizi ya Rolly kuhusu safari ya kwenda Uswidi

Rollys berättelse om resan till Sverige – swahili

Unaweza kusoma kuihusu kwenye ukurasa huu:

  • Uzoefu wa Rolly wa kuhamia nchini Uswidi.
  • Safari ya ndege kwenda Uswidi.
  • Mapokezi kwenye uwanja wa ndege.
  • Nyumba mpya.
  • Misimu tofauti na hali ya hewa.

Rolly na watoto waliotajwa kwenye barua ni wahusika wa kubuni.

Habari!

Jina langu ni Rolly na nina umri wa miaka kumi. Ninaishi katika sehemu ya kaskazini mwa Uswidi pamoja na familia yangu. Tulihamia hapa kutoka Kongo nilipokuwa na umri wa miaka saba. Tulisafiri kwa ndege. Nilifikiri ingekuwa jambo la kufurahisha na kusisimua, kwani ilikuwa mara yangu ya kwanza kusafiri kwa ndege. Kila kitu kilikwenda vizuri, chakula kilikuwa kizuri na nililala nilipokuwa kwenye ndege. Ni muhimu kuwasikiliza wazazi wako na wafanyakazi kwenye uwanja wa ndege na kwenye ndege.

Tulipofika nchini Uswidi, tulikutana na watu katika uwanja wa ndege waliotupeleka kwenye nyumba yetu mpya. Tulisafiri kwa gari kwa muda mrefu kabla ya kufika tulikokuwa tukienda. Tulipitia miji kadhaa lakini pia misitu mingi. Sijawahi kuona misitu mingi hivyo!

Mwonekano kutoka kwenye ndege.

Mwonekano kutoka kwenye ndege. Picha: Shirika la Uhamiaji la Uswidi (Migrationsverket, The Swedish Migration Agency)

Uswidi ni tofauti sana na Kongo, lakini ninapenda sana nyumba yangu mpya. Mimi pamoja na familia yangu tunaishi kwenye fleti katika ghorofa ya tatu. Ina jiko, sebule, bafu na vyumba viwili vya kulala. Mimi na dada yangu hulala katika chumba kimoja, lakini ni vigumu wakati mwingine.

Niliona kwamba majirani zangu walikuwa na mbwa aliyeruhusiwa ndani ya nyumba. Nchini Kongo, mbwa kwa kawaida huwa nje, lakini hapa Uswidi, watu wengi wana wanyama vipenzi ndani ya nyumba.

Mwanzoni nilihisi ajabu kusikia lugha ya Kiswidi ikizungumzwa kila mahali, lakini nilijifunza haraka shuleni.

Eneo la makazi ambapo majengo matatu ya ghorofa yanaonekana.

Picha: Shirika la Uhamiaji la Uswidi (Migrationsverket, The Swedish Migration Agency)/Björn Bjarnesjö

Watoto wawili wanacheza kwenye uwanja wa shule. Msichana ananing'inia mgongoni mwa mvulana.

Picha: Ann-Sofi Rosenkvist/imagebank.sweden.se

Niko katika darasa la nne. Shule ilikuwa ngumu mwanzoni kwa sababu sikuelewa Kiswidi, lakini sasa sina ugumu wa kuelewa masomo. Walimu wangu wananisaidia sana na ninaweza kuwauliza chochote kinachonitatiza. Kuna muuguzi shuleni, kwa hivyo nikiugua katika siku ya shule, ninaweza kwenda kwa muuguzi ili kupata msaada.

Nina marafiki wengi shuleni. Rafiki ninayempenda zaidi anaitwa Maja. Pia anapenda soka na huwa tunacheza pamoja wakati wa mapumziko.

Watoto wawili waliovalia ovaroli wanavuta sleji juu ya kilima kilichofunikwa na theluji.

Picha: Carolina Romare/imagebank.sweden.se

Wakati mwingine ninatamani sana kwenda nyumbani, hasa katika majira ya baridi wakati kuna baridi. Kunaweza kuwa baridi sana hapa na mara nyingi theluji hunyesha. Maja na marafiki zangu wengine wamenionyesha jinsi ya kuendesha sleji thelujini ni inafurahisha sana.

Ukivaa nguo za nje zenye joto, kwa mfano ovaroli, hutahisi baridi unapocheza kwenye theluji. Mara nyingi hupata joto kidogo!

Mkate mdogo wa mdalasini kwenye sahani na kikombe cha kinywaji moto karibu nayo.

Picha: Alexander Hall/ /imagebank.sweden.se

Baada ya kucheza kwenye theluji, mara nyingi huwa tunaingia ndani na kula "vitafunio". Fika inamaanisha kunywa maziwa, chokoleti moto au juisi na kula kuki au mikate midogo pamoja na marafiki. Napenda mikate midogo ya mdalasini, ambayo ni ya kawaida sana nchini Uswidi.

Mtoto anaruka majini kutoka kwenye gati wakati wa machweo.

Picha: Clive Tompsett/imagebank.sweden.se

Nchini Uswidi kuna misimu minne: majira ya kuchipua, joto, kupukutika kwa majani na baridi. Msimu ninaopenda zaidi ni majira ya joto. Kuna joto na jua na jambo bora zaidi ni kwamba ninaweza kuvaa fulana na suruali fupi na kucheza soka nje. Katika majira ya joto tuna mapumziko ya majira ya joto ya muda mrefu kutoka shuleni. Ninatumia wakati mwingi na marafiki zangu nje nikicheza na kuogelea. Nilipokuja nchini Uswidi sikuweza kuogelea na nililazimika kutumia jaketi ya kuokoa uhai nilipokuwa majini. Sasa nimekuwa nikienda shule ya kuogelea na nimekuwa nikiogelea kama sehemu ya elimu ya mazoezi shuleni, kwa hivyo ninajua jinsi ya kuogelea.

Hapa, pamoja na mtu mzima unaweza kusoma kuhusu jinsi ya kuogelea kwa usalama (kwa Kiswidi) External link, opens in new window.

Tunaishi karibu na ziwa. Kwa kawaida huwa tunaenda huko kuogelea na kula aiskrimu. Katika majira ya joto, jua huwaka hadi jioni. Mwanzoni ilikuwa vigumu kupata usingizi kwa sababu kulikuwa na mwangaza nje.

Mwishoni mwa Juni ni katikati ya majira ya joto na unaweza kuona bendera ya Uswidi kila mahali na katika milingoti ya katikati ya majira ya joto. Mlingoti wa katikati ya majira ya joto umefunikwa kwa majani na maua na watu kwa kawaida hucheza dansi karibu nayo. Tunachoma soseji na marafiki na kucheza. Mkesha wa Katikati ya Majira ya Joto ndiyo siku ndefu zaidi ya mwaka na sisi watoto kwa kawaida huchelewa kulala.

Karibu Uswidi, natumaini utafurahia kuwa hapa!

Rolly

Kundi la watu wanaosherehekea katikati ya majira ya joto kwa kucheza dansi karibu na mlingoti wa katikati ya majira ya joto.

Picha: Conny Fridh/imagebank.sweden.se

Maswali ya kufikiria na kuzungumzia:

  • Ulipenda nini kuhusu barua ya Rolly?
  • Unaweza kuogelea? Unajua jinsi ya kuoga kwa usalama?
  • Kuna kitu chochote kwenye barua hiyo kilichokuwa kipya kwako?

Last updated: