Simulizi ya Solomon kuhusu mila ya Uswidi

Solomons berättelse om svenska traditioner – swahili

Unaweza kusoma kuihusu kwenye ukurasa huu:

  • Sherehe ya Lucia.
  • Krismasi nchini Uswidi.
  • Chakula cha kawaida nchini Uswidi.

Solomon na watoto waliotajwa kwenye barua ni wahusika wa kubuni.

Habari!

Jina langu ni Solomon na nina umri wa miaka 9. Hapa Uswidi kuna mila nyingi ambazo ni tofauti na ile niliyozoea kusherehekea na familia yangu nchini Eritrea. Mwanzoni, mila nyingi za Uswidi zilikuwa geni kwangu, lakini nilifurahia kujifunza kuzihusu.

Jana, kwa mfano, tulisherehekea Lucia shuleni. Ilifurahisha sana! Darasa langu lilikuwa na onyesho la Lucia ambapo sote tulivalia mavazi maalum na kuimba nyimbo. Nilikuwa nimevaa kama kibwengo.

Baadaye tulipata chokoleti moto na "mkate mdogo wa zafarani". Lussekatt ni mkate mdogo wa njano unaofanana na herufi S, na nadhani ulikuwa mtamu!

Hata ingawa mimi hutumia kiti cha magurudumu, ninaweza kuwa sehemu ya sherehe ya Lucia. Ilinifurahisha. Nchini Uswidi, inawezekana kufika karibu kila mahali ukiwa kwenye kiti cha magurudumu. Inafanya kila kitu kiwe shwari kidogo kwangu na ninaweza kushiriki katika shughuli nyingi.

Watoto watano wameketi mezani wakiwa na mavazi ya Lucia na Santa na wanakula mikate midogo ya zafarani, mkate wa tangawizi na machungwa.

Picha: Emelie Asplund/imagebank.sweden.se

Baada ya Lucia, ni karibu na Krismasi. Nchini Uswidi, watu wengi husherehekea Krismasi, hata wale ambao hawaamini Mungu.

Wakati wa Krismasi, kwa kawaida wewe hutumia wakati pamoja na familia yako, kula chakula maalum cha Krismasi na kupeana zawadi za Krismasi. Kisha tunapata mapumziko ya wiki mbili kutoka shuleni.

Pia huwa tunaoka kuki za mkate wa tangawizi na kunywa julmust, ambayo ni aina ya kinywaji kisicholewesha.

Watoto watatu wanaoka kuki za mkate wa tangawizi pamoja.

Picha: Lena Granefel/imagebank.sweden.se

Sahani iliyo na viazi vilivyopondwa, mipira ya nyama, lingonberry na tango yenye achari.

Sahani iliyo na viazi vilivyopondwa, mipira ya nyama, lingonberry na tango yenye achari. Picha: Lieselotte van der Meijs/imagebank.sweden.se

Ilinichukua muda kuzoea chakula cha Uswidi, lakini sasa nakipenda. Hapa mtu hula viazi vingi pamoja na nyama au samaki. Nyumbani bado tunakula chakula cha Eritrea, lakini pia tumeanza kula chakula cha Uswidi. Nadhani vyote viwili ni vizuri!

Je, wajua kwamba Uswidi ina mfalme na malkia? Lakini hawaruhusiwi kufanya maamuzi, kama ilivyo katika baadhi ya nchi nyingine. Mfalme na malkia wanaishi katika mji mkuu wa Stockholm.

Drottningholm Palace, makazi ya kibinafsi ya familia ya kifalme. Picha inaonyesha kasri lenye msitu unaolizunguka na ziwa kubwa mbele yake.

Drottningholm Palace, makazi ya kibinafsi ya familia ya kifalme. Picha: Melker Dahlstrand/imagebank.sweden.se

Katika wikendi ninakutana na marafiki zangu. Wikendi hii nitakutana na rafiki yangu Rolly. Tunaenda kwenye sinema.

Solomon

Maswali ya kufikiria na kuzungumzia:

  • Una maoni gani kuhusu barua ya Solomon?
  • Umewahi kusikia kuhusu Lucia hapo awali?
  • Je, huwa unasherehekea sikukuu zozote katika familia yako?
  • Una vyakula vyovyote unavyokula katika matukio maalum pekee?

Last updated: